slide 1
slide 1
Image Slide 2
Asali ya Rawza
Image Slide 2
Kahawa
previous arrowprevious arrow
next arrownext arrow
Shadow

Asali na Kahawa

Asali na kahawa ni miongoni mwa njia bora za urembo wa asili usio na madhara, faida za kutumia asali na kahawa huonekana muda mfupi baada ya mtumiaji kuanza kuvitumia.

Ni muhimu kuhakikisha unatumia asali mbichi halisi 100%, matumizi ya asali iliyochakachuliwa huweza kukuletea madhara makubwa katika ngozi yako. Kununua asali ya Rawza wasiliana nasi kwa namba ya simu 0787001819.

FAIDA ZA ASALI

Kwa urembo wa uso

KUSAFISHA NGOZI

Rawza Honey ina properties za antibakteria na antifangasi, ambazo zinaweza kusaidia kusafisha ngozi kwa kuondoa vijidudu na vimelea vinavyosababisha matatizo ya ngozi.

KULINDA NGOZI

Asali mbichi ya Rawza ina antioxidants za asili, ambazo zinaweza kusaidia kulinda ngozi dhidi ya uharibifu wa seli za ngozi. Jambo hili huifanya ngozi kuwa na afya na yenye kung’aa muda wote.

KUNG'ARISHA NGOZI

Rawza Honey ni kioevu chenye  uwezo wa kushikilia kiwango cha unyevu kwenye ngozi. Hii inasaidia ngozi kuwa laini, yenye unyevu na yenye kung’aa kwa kuwa na kiwango cha unyevu kinachofaa. 

Asali na Kahawa

Asali ya Rawza na Kahawa

Jinsi ya kuandaa maski ya Asali ya Rawza na Kahawa ya unga (isiyoongezewa kemikali).

 

Vifaa Vinavyohitajika

• Vijiko viwili vya asali ya Rawza

• Vijiko viwili vya kahawa

• Bakuli dogo na kijiko cha kuchanganyia

 

Hatua za Kuandaa

1. Anza kwa kuweka vijiko 2 vya asali katika bakuli lako dogo.

2. Ongeza vijiko 2 vya kahawa kwenye bakuli, changanya vizuri hadi kupata mchanganyiko laini.

3. Baada ya kuchanganya vizuri, maski yako ya asali ya Rawza na kahawa itakuwa tayari kwa kutumika.

 

Jinsi ya Kutumia

1. Osha uso wako vizuri kwa maji safi na sabuni, kisha ukaushe kwa taulo.

2. Paka maski yako usoni kwa kutumia brashi laini au vidole, ukitoa tahadhari ya kuepuka eneo la ndani ya macho.

3. Weka tabasamu kwenye uso wako, ili kuzuia misuli ya uso kujifunga wakati maski inakauka.

4. Acha maski ikae usoni kwa takriban dakika kama 15-20 ili viungo vyake viweze kufanya kazi katika ngozi yako.

5. Baada ya muda uliopita, osha uso wako kwa maji ya uvuguvugu na upake moisturizer ikiwa unataka.

 

ANGALIZO:

1. Hakikisha unatumia asali mbichi ya Rawza, matumizi ya asali isiyo mbichi au isiyochujwa vizuri huweza kukuletea matatizo kwenye ngozi.

2. Jaribu kutumia aina maski hii katika sehemu ndogo ya ngozi kuona kama itakukubali, hii ni kanuni muhimu kwa kila aina ya maski ya uso.

Bofya Kitufe Kuwasiliana Nasi

Scroll to Top